<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>39</hymn_number>
<lyrics>[V1]
 Mwenye dhambi huna raha,
 Sikiza nakusihi,
 Utapata msamaha
 Kwake Yesu Mwokozi!
 Njoo hima, njoo hima,
 Naye atafurahi.

[V2]
 Yesu anakwita sana
 Naye yuko Mbinguni;
 Hofu ya kifo hapana
 Kwake ukiamini.
 Njoo hima, njoo hima,
 Utapata amani.

[V3]
 Hatakwita siku zote;
 Ni ya sasa nafasi.
 Lete na uchafu wote,
 Kukawa haipasi.
 Njoo hima, njoo hima,
 Ni wokovu halisi.

[V4]
 Uzima uko kwa Bwana
 Twae uzima hasa
 Bure unapatikana,
 Wokovu twae sasa!
 Njoo hima, njoo hima,
 Twae utakatifu.</lyrics>
<title>Mwenye Dhambi Huna Raha TZR39</title>
</song>